Walimu 380 wanafundisha katika semina za Qur’ani za majira ya kiangazi katika mji wa Baabil.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imesema kuwa, walimu (380) wanafundisha semina za Qur’ani za majira ya kiangazi katika mji wa Baabil.

Kiongozi wa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa Sayyid Muntadhar Mashaikhi amesema “Mwaka huu Maahadi imepokea zaidi ya wanafunzi 10,000 wanaoshiriki kwenye semina za majira ya kiangazi chini ya walimu 380”.

Akaongeza kuwa “Maahadi iliandaa walimu 380 kupitia warsha na semina za kuwajengea uwezo katika mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni mbinu za ufundishaji, Fiqhi, Aqida, Akhlaq na mihadhara mbalimbali kuhusu malengo ya semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi”.

Akaendelea kusema kuwa “Asilimua kubwa ya walimu wa semina za Qur’ani katika majira ya kiangazi ni wahitimu wa Maahadi, jambo hilo limerahisisha kupanua wigo wa semina kwenye maeneo mengine ya mkoa wa Baabil, na wengine ni wanafunzi wa Dini walioandaliwa rasmi na Maahadi kwa ajili ya kushiriki kwenye mradi huu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: