Wakazi wa Karbala wameipongenza Atabatu Abbasiyya kwa kuhudumia mazuwaru wa mji huo mtukufu.

Wakazi wa Karbala wameipongeza Atabatu Abbasiyya kwa namna inavyohudumia mazuwaru wa mji huo na kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).

Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini amesema “Pongezi za wakazi wa Karbala kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, zinatokana na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), mawakibu na vikundi vya Husseiniyya”.

Mmoja wa watu wa Karbala Sayyid Liith Hamdu Kishwani amesema “Pongezi za Atabatu Abbasiyya tukufu zimetolewa na wakazi wa mji wa Karbala kutokana na huduma nzuri zinazotolewa na Ataba kwa mazuwaru na wakati wa kuhuisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).

Akaongeza kuwa “Tunatoa shukrani za dhati kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini kwa juhudi kubwa wanayofanya katika kuhudumia mazuwaru na mji wa Karbala kwa ujumla”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: