Ugeni kutoka Ataba umehusisha vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu, shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi tofauti wa Dini, wawakilishi wa hauza, wawakilishi wa Ataba na wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Ukumbi wa haram ya Alkaadhimiyya umeshuhudia shughuli ya kubadili bendera za kubba mbili za Maimamu wa wili Aljawadaini (a.s), na kuwekwa bendera nyeusi zinazoashiria huzuni kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) aliyefariki mwezi thelathini Dhulqaadah.
Shughuli imefanywa katika mazingira ya kiimani yaliyojaa huzuni kufuatia msiba huo mkubwa na mateso aliyopitia Imamu (a.s).