Atabatu Abbasiyya imeweka mabango yanayoashiria huzuni kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Aljawaad (a.s).

Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram katika Atabatu Abbasiyya, wameweka mabango wanayoashiria huzuni na majonzi ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Zainul-Aabidina Quraishi amesema “Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wameweka mabango yanayo ashiria huzuni na majonzi, yaliyotengenezwa maalum kwa kila sehemu za haram, kwenye kuta na milango”.

Akaongeza kuwa “Vitambaa na mabango yanayoashiria huzuni yamewekwa kwenye nguzo na kuta za Ataba, huku vitambaa vikubwa vikiwekwa kwenye kuta na milango ya nje”.

Akabainisha kuwa “Kazi ya kuweka vitambaa na mabango hufanywa kwa umaridadi mkubwa, huwekwa kwa kutumia gundi maalumu ambayo haiathiri ukuta, mabango yameandikwa na kudariziwa jumbe mbalimbali zinazo ashiria huzuni na majonzi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: