Atabatu Abbasiyya tukufu imepokea msafara wa kushindikiza muili wa Allamah Shekhe Muhammad Ridha Alqaini Annajafi mmoja wa viongozi wa hauza na walimu wa Najafu tukufu.
Muili wa Allamah Alqaini umeingizwa katika ukumbi wa haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mbele ya kundi kubwa la walimu wa hauza, wanafunzi, wawakilishi wa Maraajii watukufu, waumini na wahudumu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Shekhe Muhammad Ridha bun Shekhe Muhammad Hussein bun Shekhe Abdurazaaq Alqaini Annajafi alizaliwa katika mji wa Najafu, na kulelewa katika familia ya kielimu.