Sayyid Swafi akutana na walimu wa mradi wa Jaamiu-Twarihi wa Qur’ani na Fiqhi katika mji wa Najafu.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi amekutana na viongozi wa mradi wa Qur’ani na Fiqhi pamoja na walimu wao katika mji wa Najafa, na baadhi ya wanafunzi wa mradi huo.

Mkuu wa mradi Shekhe Muhammad Khafaji ameeleza ratiba ya mradi na malengo yake ya kuandaa vijana wenye kufuata maadili bora ya Dini na utamaduni, wanaoweza kupambana na changamoto za jamii, watakaoishi kwa kufuata maadili ya mji mtukufu wa Najafu, mradi unalenga idadi kubwa ya wanafunzi wa hauza na walimu wao katika mji wa Najafu.

Sayyid Swafi akasikiliza usomaji wa baadhi ya wanafunzi, kuna waliosoma Qur’ani kwa kuhifadhi, Khutuba za Nahaju-Balagha na Hadithi, amewapongeza washiriki kwa namna walivyo hifadhi Qur’ani, Nahaju-Balagha na Hadithi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: