Kiongozi wa idara Bibi Fatuma Mussawi amesema “Semina imegawanyika sehemu mbili kulingana na umri wa washiriki, wenye umri mkubwa wanasoma Jumapili na Jumatatu, na wenye umri mdogo wanasoma Jumanne na Jumatano, semina inatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi wa saba”.
Akaongeza kuwa “Wanafundishwa masomo tofauti, miongoni mwa masomo hayo ni Fiqhi, Aqida, Akhlaq, visa vya Qur’ani na kazi za mikono, aidha wanapewa mihadhara ya kimaadili kulingana na umri wao”, akabainisha kuwa “Tumeandaa safari za kimatembezi kwa washiriki wa semina zote mbili”.
Semina hizi ni sehemu ya kutumia vizuri wakati wa likizo za majira ya kiangazi, aidha ni sehemu ya harakati za idara inayolenga kuwajenga wanafunzi kimaadili na kuwafungamanisha na vizito viwili vitakatifu.