Idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya, inaendelea na majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).
Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na itadumu kwa muda wa siku tatu, asubuhi na jioni kila siku.
Wahadhiri wameeleza historia ya Imamu Aljawaad (a.s), wakati wa utawala wa bani Abbasi, aidha wamehimiza kufuata mwenendo wake katika kuvumilia na kutekeleza majukumu katika umma na Dini tukufu ya kiislamu sambamba na kuhudumia binaadamu wote.
Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi katika kuomboleza msiba huo.