Maukibu imeanza matembezi yake katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kusimama kwa mistari kisha ikaelekea katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) kwa kupita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wakiimba maneno ya kuomboleza na kuhuzunisha yaliyo amsha majonzi katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Matembezi hayo yakaishia ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlisi ya kuomboleza, ambapo wahudumu wa Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya wameshiriki pamoja na mazuwaru, katika Majlisi hiyo zimesomwa qawsida na tenzi za kuomboleza.
Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, hufanya maukibu ya pamoja katika kuomboleza matukio ya Ahlulbait (a.s) wakati wote wa mwaka.