Sayyid Swafi amzawadia mmoja wa waliojitolea katika kuitikia wito wa fatwa ya jihadi kifaya.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, amekabidhi zawadi kwa mmoja wa walioitikia wito wa fatwa ya jihadi kifaya.

Amefanya hivyo alipompokea mmoja wa wapiganaji wa kikosi za Abbasi (a.s) Shekhe Qassim Aljaburi, aliyeshiriki kwenye vita ya kuikomboa Iraq dhidi ya magaidi.

Akatoa wito wa kuwajali wapiganaji, kwani wao ndio walioleta amani ya taifa la Iraq, wao ni watoto wa Marjaa Dini mkuu walioitikia wito wa fatwa ya jihadi kifaya, iliyotolewa na Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani.

Sayyid Swafi akapongeza kujitolea kukubwa kwa wale walioitikia wito wa fatwa ya jihadi kifaya katika kulinda ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu, na msimamo wao Madhubuti kuhusu fatwa ya jihadi kifaya iliyotolewa na Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu dhidi ya magaidi wa Daeshi.

Aljaburi amesema “Leo tumekutana na Muheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, baada ya kupata agizo la kushiriki kwenye mradi wa kufuta ujinga (elimu ya watu wazima) kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s), ndani ya mwaka mmoja na miezi mitatu sasa hivi kikosi hakina mjumbe asiyejua kusoma na kuandika, ndani ya kipingi hicho zaidi ya wajumbe 1000 wamejua kusoma na kuandika”.

Akaongeza kuwa “Leo nimeitwa kuja kutunukiwa cheti cha shukrani, jambo hili limenitia moyo kutokana na majeraha niliyopata vitani pale niliposhambuliwa risasi nyingi na magaidi wa Daeshi”.

Aljaburi akatoa shukrani nyingi kwa kiongozi mkuu wa kisheria kwa msaada anaopata kutoka kwake pamoja na wenzake walioitikia wito wa fatwa tukufu na kuhuisha utii wao kwa Marjaa Dini mkuu kupitia kulinda taifa la Iraq na raia wake.

Siku hizi zinasadifu kumbukizi ya miaka nane tangu vita vya ukombozi wa Iraq dhidi ya magaidi wa Daeishi kupiganwa, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanywa kongamano la kuadhimisha fatwa tukufu ya jihadi kifaya, kongamano hilo limedumu kwa muda wa siku mbili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: