Mahafidhu wa Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, wameshiriki kwenye hafla ya usomaji wa Qur’ani katika Atabatu Radhawiyya.
Walioshiriki kwenye hafla hiyo ya usomaji wa Qur’ani ni wanafunzi wa Maahadi ya Qur’ani kutoka Najafu chini ya Majmaa, wakiongozwa na Muhammad Jawaad Banahi.
Ushiriki huo umetokana na ratiba ya kutembelea Ataba takatifu katika nchi ya Iran, inayohusisha wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo yao.
Ushiriki umehusisha kujibu maswali yanayohusu Qur’ani na kusoma kwa kuhifadhi sehemu wanazotajiwa mbele ya umati mkubwa wa wahudhuriaji.