Idara ya Dini tawi la wanawake imeomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Kiongozi wa Idara Bibi Adhraa Shami amesema, “Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu na ziara ya Imamu Aljawaad (a.s), ukafuata muhadhara kutoka kwa mmoja wa wahadhiri wenye anuani isemayo (Mfumo wa Imamu Aljawaad -a.s- katika Islahi).

Akaongeza kuwa “Majlisi imepambwa na qaswida na ikahitimishwa kwa Dua ya Faraj, ndani ya sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: