Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake katika jiji la Baghdad chini ya Atabatu Abbasiyya, imefanya hafla ya kuadhimisha ndoa ya Imamu Ali (a.s) na Bibi Fatuma Zaharaa (a.s).
Kiongozi wa tawi Bibi Anwaru Abdurazaaq amesema “Hafla imepambwa na muhadhara ulioeleza kisa cha ndoa hiyo tukufu, na matunda ya ndoa hiyo ambayo yanaendelea kunufaisha waumini hadi leo, kwa kupatikana Maimamu watakasifu, wanachuoni, wapokezi wa hadithi na kuwa hoja juu yetu”.
Akaongeza kuwa “Hafla imehusisha usomaji wa Qur’ani na mambo mengine zikiwemo tenzi na mashairi yaliyoamsha hisia za furaha kutokana na tukio hilo”.
Hafla hiyo ni sehemu ya harakati za Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la wanawake, kwa lengo la kukuza uwelewa wa Dini kupitia kuadhimisha matukio muhimu ya kidini katika nafsi za waumini.