Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake inaonyesha machapisho ya Atabatu Abbasiyya.

Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya, imeonyesha baadhi ya machapisho ya Ataba tukufu kwenye maonyesho ya biashara yanayofanyika kwa mara ya kwanza.

Maonyesho hayo yanafanywa kwenye jengo la kibiashara la Al-Afaaf, bidhaa mbalimbali za kutengenezwa kwa mikono zinashiriki.

Kiongozi wa maktaba Bibi Nuru Ali amesema “Maktaba imeonyesha baadhi ya vitabu vya Ataba katika ushiriki wake kwenye maonyesho hayo”, akaongeza kuwa “Vitabu vinavyo onyeshwa vimeshiba mada muhimu katika jamii, vimeandika mambo ya kidini na mengineyo”.

Akasema “Vitabu vimepata muitikio mkubwa kotoka kwa wadau wa maonyesho, wamevutiwa sana na mada zilizomo kwenye vitabu vinavyo onyeshwa na tawi la maktaba ya Ummul-Banina (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: