Kamati kuu ya kuhuisha turathi inafanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa Maahadi ya Turathi.

Kamati kuu ya kuhuisha turathi katika Atabatu Abbasiyya imefanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi wa Maahadi ya turathi chini ya kamati.

Mkuu wa Maahadi Sayyid Abdulhakiim Swafi amesema “Kamati kuu ya turathi imefanya mitihani ya mwisho kwa wanafunzi (30), imehusisha mada zote walizosoma kwa muda wa miezi mitatu”.

Akaongeza kuwa “Mitihani imehusisha mada tofauti, miongoni mwa mada hizo ni kuhakiki nyaraka, faharasi ya nakala-kale, mada ya imla na tarqidi yenye umuhimu mkubwa katika kushepu nakala na kuikata, mfumo wa tafiti za kielimu katika turathi, ambao huhitajiwa na mhakiki katika kuandika utangulizi wa utafiti, nao ni muhimu katika uandishi kwani huchukuliwa kama mlango unaomtambulisha mhakiki”.

Akaendelea kusema “Maahadi ya turathi iliweka mazingira mazuri ya mitihani”, akasema “Wakati wa kila mtihani ni saa tatu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: