Ratiba ya siku ya kwanza ya kongamano la kielimu la fatwa ya kujilinda jihadi kifaya linalosimamiwa na kikosi cha Abbasi (a.s) imekamilika.
Kongamano linafanywa kwa kushirikiana na kitivo cha sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Baghdad chini ya Atabatu Abbasiyya, kufuatia kufika miaka kumi tangu ilipotolewa fatwa ya kujilinda jihadi kifaya, chini ya kauli mbiu isemayo (Jihadi kifaya imefungamana na utoaji na ujenzi) kuanzia tarehe 11 – 12/ 6/ 2024m.
Ratiba ya siku ya kwanza imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, wajumbe wa kamati kuu na baadhi ya viongozi wa kisekula.
Kongamano la kielimu linamada (48) zitakazo wasilishwa kupitia vikao (8), miongoni mwa mada hizo ni (Marjaiyya Diniyya na ujenzi wa taifa la Iraq, Fatwa ya kujilinda jihadi kifaya na usalama wa jamii, Fatwa ya kujilinda jihadi kifaya na mwitikio wa wananchi, Fatwa ya kujilinda jihadi kifaya na ujenzi wa amani, Marjaiyya Diniyya na umoja wa kitaifa, Marjaiyya Diniyya na mabadiliko ya demokrasia nchini Iraq, Marjaiyya Diniyya na maendeleo endelevu, Fatwa ya kujilinda jihadi kifaya na Marjaiyya Diniyya, Muitikio wa ndani na nje katika kusapoti siasa za Iraq na utulivu wake, kila mada inatafiti (6) za kielimu.
Atabatu Abbasiyya inaendelea kufafanua umuhimu wa fatwa tukufu ya kujilinda katika kupambana na changamoto, na nafasi yake katika kulinda taifa na kuimarisha usalama katika jamii, aidha kongamano linahimiza kuzingatia elimu ikiwa kama njia ya kujenga mustaqbali bora wa Iraq.