Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya amesema: Mada zinazowasilishwa katika kongamano la fatwa ya kujilinda jihadi kifaya zinachangia kuimarisha amani katika jamii.

Mkuu wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Dokta Afdhalu Shami amesema kuwa, mada zinazowasilishwa katika kongamano la kielimu kuhusu fatwa ya kujilinda jihadi kifaya, zinachangia kuimarisha usalama katika jamii.

Kikosi cha Abbasi (a.s) kinafanya kongamano hilo kwa kushirikiana na kitivo cha sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha Baghdad chini ya kauli mbiu isemayo (Fatwa ya kujilinda jihadi kifaya inafungamana na utoaji na ujenzi).

Akasema: “Mada za kongamano kuhusu nafasi ya Marjaiyya Diniyya na fatwa ya kujilinda jihadi kifaya, zinasaidia kuimarisha usalama katika jamii ndani ya Iraq, fatwa imefundisha namna ya kuimarisha amani katika jamii”, akasema kuwa “Wazungumzaji wameeleza dalili za kuthibitisha hilo”.

Akaongeza kuwa “Fatwa tukufu iliitikiwa na makundi ya watu tofauti katika raia wa Iraq, walioshiriki kukomboa sehemu zilizokuwa zimetekwa na magaidi wa Daesh, jambo hilo linaimarisha usalama wa jamii, sambamba na maelekezo ya Marjaiyya Diniyya kwa wapiganaji, ambapo aliendelea kuhimiza ulazima wa kuheshimu wananchi na mali zao katika maeneo waliyokomboa”. Akasema “Kongamano limehimiza ulazima wa kuenzi jambo hilo, kwa ajili ya kuimarisha amani katika jamii na kuendeleza malengo ya fatwa tukufu”.

Akabainisha kuwa “Kwa ujumla tunatarajia kongamano hili litaimarisha uwelewa wa yaliyotokea kupitia mada zinazowasilishwa na kutekeleza wajubu wetu katika fatwa hiyo tukufu, jamii yetu na vizazi vijavyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: