Idara ya Dini tawi la wanawake inaendelea na semina za lugha ya kifarsi kwa watumishi wake

Idara ya Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, inafanya semina ya lugha ya kifarisi kwa watumishi wake.

Kiongozi wa idara Bibi Adhraa Shami amesema “Idara inaendelea na semina za kufundisha lugha ya kifarsi kila siku ya Jumanne ndani ya Sardabu ya Alqami katika Ataba tukufu, wanafundishwa kusoma, kuandika na kuongea lugha ya kifarsi”.

Akaongeza kuwa “Semina imeandaliwa na (Amina Mussawi) kutoka idara ya maswali ya kisheria, kutakuwa na mitihani ya kuongea na kuandika kwa lengo la kupima uwezo wa washiriki”.

Washiriki wa semina hiyo wameonyesha kufurahishwa na wanachofundishwa, wamesema itawasaidia kuongeza uwezo wa kuongea lugha hiyo na kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa kike wanaotumia lugha hiyo katika mji wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: