Miongoni mwa kazi zake za kitablighi.. kitengo cha habari na utamaduni kimefanya program ya kitamaduni nchini Naijeria.

Kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya program ya kitamaduni nchini Naijeria.

Program hiyo imesimamiwa na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya kitengo.

Kiongozi wa idara ya Tablighi katika Markazi, Sayyid Muslim Aljaabiri amesema “Program inalenga kuwatambulisha vijana na wanafunzi historia ya Ahlulbait (a.s) kwa lengo la kuimarisha uwelewa wa Dini na misingi ya kiislamu”.

Akaongeza kuwa “Program imeratibiwa kupitia muwakilishi wa Markazi Shekhe Muhammad Abdullah Twaibu kwenye madrasa ya Imamu Swadiq (a.s) katika mji wa Nasrawi nchini Naijeria”.

Akabainisha kuwa “Program imepambwa na vikao vya kielimu ambapo wameongelewa kwa kina Ahlulbait (a.s) na kutolewa kwa nafasi ya kuuliza maswali, jambo ambalo limesaidia kufikia malengo”.

Akafafanua kuwa “Markazi hufanya program mbalimbali kwa lengo la kufundisha mwenendo wa Ahlulbait (a.s) katika jamii sambamba na kuimarisha misingi ya uislamu kwa vijana”.

Program hiyo ni sehemu ya harakati zinazofanywa na Markazi Dirasaati Afriqiyya katika bara la Afrika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: