Siku ya pili.. Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Albaaqir (a.s).

Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) kwa siku ya pili mfululizo.

Majlisi imesimamiwa na idara ya wahadhiri chini ya Ataba, nayo ni sehemu ya harakati za uombolezaji wa Atabatu Abbasiyya katika kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s).

Mzungumzaji wa Majlisi alikuwa Shekhe Hussein Farahani, ameongea kuhusu historia ya Imamu Albaaqir (a.s) sambamba na kubainisha elimu na uchamungu wake, Pamoja na kuangazia mafunzo na mazingatio katika Maisha yake (a.s).

Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalum yenye vipengele vingi katika kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: