Kupitia majlisi ya kuoboleza.. Atabatu Abbasiyya imeomboleza kifo cha Imamu Albaaqir (a.s)

Atabatu Abbasiyya imefanya Majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s).

Majlisi imehudhuriwa na wahudumu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ukumbi wa utawala ndani ya Ataba tukufu, katika mazingira yaliyojaa huzuni kutokana na ukubwa wa msiba huo katika nafsi za waumini.

Mhadhiri wa Majlisi Sayyid Aadil Ashkanani amesema “Majlisi iliyofanywa ndani ya Ataba tukufu ilikuwa na anuani isemayo (Imamu Albaaqir -a.s- na utengenezaji wa umma), amefafanua maana ya utengenezaji na jinsi ya kufanyia kazi”.

Akaendelea kusema “Majlisi ilikuwa na vipengele tofauti, historia ya Imamu Albaaqir (a.s), kubainisha ukubwa wa elimu yake, mafundisho yanayopatikana katika Maisha yake na ikahitimishwa kwa kusoma tenzi zinazomuhusu Imamu Muhammad Albaaqir (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huo, yenye vipengele tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: