Mawakibu nyingi za watu wa Karbala, zimekuja kutoa pole kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kumbukizi ya kifo cha Imamu Albaaqir (a.s).
Matembezi ya kuomboleza ni utamaduni uliozoweleka kwa watu wa Karbala kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuomboleza tukio la kifo cha Ahlulbait (a.s).
Mshairi Ghasani Quraishi kutoka kwenye moja ya mawakibu za kuomboleza amesema “Maukibu ya kuomboleza huanza matembezi yake katika eneo la Baabu-Baghdad na huishia kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s)” akaongeza kuwa “Mawakibu za kuomboleza zimetoa pole ya msiba huo wa kifo cha Imamu Albaaqir (a.s)”.
Akaendelea kusema “Mawakibu huenda kutoa pole katika haram mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil (a.s) katika kila tukio la kumbukizi ya kifo cha Ahlulbait (a.s)”.
Mshairi mwingine Farasi Asadi kutoka maukibu ya watu wa Karbala amesema “Matembezi ya kuomboleza yanayofanywa na watu wa Karbala wamerithi kwa mababu na mababu, toka zamani watu wa Karbala walikuwa na utamaduni wa Kwenda kutoa pole katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.