Wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wanaomboleza kifo cha Imamu Muhammad Albaaqir (a.s) kupitia maukibu ya pamoja.
Maukibu imeanza matembezi yake ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha wakaelekea kwenye malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakipita katikati ya uwanja wa baina ya haram mbili tukufu, huku wanasoma tenzi na mashairi ya kuomboleza, yaliyoamsha hisia za majonzi katika nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s).
Matembezi yameishia ndani ya haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya Majlisi ya kuomboleza, ambayo watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wameshiriki pamoja na kundi kubwa la mazuwaru.
Ni desturi ya wahudumu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika mji wa Karbala, kufanya maukibu ya pamoja katika kuadhimisha matukio yanayohusu Ahlulbait (a.s).