Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi, anakagua ratiba ya msimu wa kiangazi katika shule za Al-Ameed.
Amefanya hivyo alipotembelea kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya na kupokewa na rais wa kitengo hicho Dokta Hassan Daakhil Hasanawi, makamo wake Sayyid Yusufu Twaaiy na mkuu wa shule za wavulana za Al-Ameed Dokta Haidari A’raji.
Sayyid Swafi amepewa maelezo kuhusu semina za majira ya kiangazi, ikiwemo ratiba ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed na ratiba ya safari za mapumziko kwa lengo la kuwajengea hamasa walimu baada ya kazi kubwa waliyofanya kwa muda wa mwaka mzima.
Sayyid Swafi akawahakikishia msaada wa Atabatu Abbasiyya kwa kitengo hicho ili kiweze kufikia malengo yake kitaaluma na kufikiwa matumaini ya wazazi na wadau wa elimu.