Makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Habibu Dahashi amesema “Watumishi wa kitengo wamejiandaa kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku ya Arafa na Idul-adh-ha”.
Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa madeli ya maji zaidi ya (15) na vipande vya barafu elfu tano kwa ajili ya kugawa kwa mazuwaru watakaokuja kufanya ibada za siku ya Arafa na Idul-adh-ha”.
Akaendelea kusema kuwa “Watumishi wetu wametandika uwanja wa Katikati ya haram zaidi ya mazulia elfu moja, kwa lengo la kusoma dua ya Imamu Hussein (a.s) ya siku ya Arafa, Pamoja na kufunga feni zinazo nyunyiza maji kwa kushirikiana na kitengo cha ujenzi na uhandisi ili kupunguza joto”.