Waumini wamefanya ziara ya siku ya Arafa mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala.
Mazuwaru wamemiminika kwa wingi kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala kuja kufanya ibada hiyo tukufu, katika mazingira tulivu na salama.
Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na maeneo yanayozunguka Atabatu Abbasiyya yamefurika waumini waliokuja kufanya ziara na ibada mbalimbali chini ya mwanga wa jua.
Idada hizi hufanywa kila mwaka katika siku ya mwezi tisa Dhulhijjah, waumini huja katika mji wa Karbala na kufanya ibada mbele ya malalo mbili takatifu.
Kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji wa ziara na ibada mbalimbali, Atabatu Abbasiyya umeweka wahudumu maalumu kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru.
Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni kuandaa sehemu za vyoo, vituo vya afya, maji safi ya kunywa, sehemu za kupumzika, kuratibu utembeaji wa mazuwaru, yote hayo yamefanywa chini ya mazingira tulivu na salama.
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa chakula cha bure na kukigawa kwa mazuwaru, aidha imetoa huduma za afya kupitia kikosi kazi maalum chenye vifaa tiba vya kisasa, yote hayo yamefanywa kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa idaba katika mazingira tulivu na salama.