Majmaa-Ilmi inatoa mihadhara ya kimalezi kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, inatoa mihadhara ya kimalezi kwa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Karbala.

Kiongozi wa idara ya kuhifadhi katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Shekhe Ali Rawii amesema, “Maahadi kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Karbala, imewashirikisha wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani katika mihadhara ya kimalezi”.

Akaongeza kuwa “Mihadhara inatolewa na wahadhiri bobezi wa chuo kikuu cha Karbala siku mbili kwa wiki, ratiba hiyo itadumu kwa muda wa miezi mitatu, inalenga kuwajenga kimaadili wanafunzi”.

Muhadhara wa kwanza umetolewa na rais wa kitengo cha lugha ya kiarabu katika chuo kikuu cha Karbala Dokta Haamid Shihaab, ameongea kuhusu uraibu wa kimtandao na ubaya wake, changamoto za teknolojia na namna teknolojia inavyo haribu vijana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: