Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekhe Swalahu Karbalai amesema, Swala ya Idul-adh-ha imeswaliwa zaidi ya mara moja ndani ya haram tukufu bila kuathiri harakati za mazuwaru, pamoja na wingi wa mazuwaru kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Akaongeza kuwa “Uwanja wa Katikati ya haram mbili umeshuhudia swala za Idi zilizoswalishwa na maimamu tofauti Masayyid na Mashekhe kutokana na wingi wa wenye kuswali waliofurika eneo lote la uwanja huo”.
Waumini wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape amani na utulivu katika taifa hili la Iraq na awarehemu mashahidi na kuwaponya haraka majeruhi.
Atabatu Abbasiyya imejiandaa kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kuwapa huduma bora kuanzia siku ya Arafa hadi siku za Idi tukufu na kuhakikisha wanafanya ibada kwa amani na utulivu.