Sayyid Swafi anapokea watu wanaokuja kutoa salama za Idul-adh-ha.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, asubuhi ya Jumatatu amepokea watu waliokuja kutoa salam ya Idul-adh-ha.

Katika kikao cha kupokea watu hao alikuwepo pia katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhiyaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu, marais wa vitengo na viongozi wa idara, wote kwa pamoja wametoa na kupokea salam za Idi kutoka kwa watu mbalimbali.

Atabatu Abbasiyya tukufu imeshuhudia viongozi wa kidini, kikabila, kijamii, kisiasa na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, wakija kutoa salam za Idul-adh-ha, sambamba na kumuomba Mwenyezi Mungu alipe amani na utulivu taifa la Iraq na raia wake.

Sayyid Swafi amemuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada za waja wote, na alinde taifa la Iraq na raia wake, awatunuku amani na usalama, ametoa shukrani za dhati kwa watu wote waliokuja kutoa salam za Idi, amewatakia kheri na mafanikio katika Maisha yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: