Shekhe Karbalai amefuatana na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya, naibu katibu mkuu, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na baadhi ya viongozi, wamekuja kutoa pongezi za Idi kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ugeni huo umepokewa wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadha Aalu Dhitaau-Dini, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu, marais wa vitengo na baadhi ya viongozi.
Wamepeana pongezi za sikukuu na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aliweke salama taifa na raia wa Iraq.
Atabatu Abbasiyya Jumatatu asubuhi imeshuhudia viongozi wengi wa kidini, kikabila, kijamii na kisiasa wakija kutoa salam za Idi, aidha waumini na mazuwaru wengi wameshiriki kwenye swala ya Idi.