Makumbusho ya Alkafeel imetembelewa na watu wengi katika siku za sikukuu ya Adul-adh-ha.

Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya, imetembelewa na watu wengi kutoka ndani na nje ya Iraq katika siku za Idul-adh-ha.

Ukumbi wa maonyesho ya makumbusho ya Alkafeel uliopo ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hufunguliwa asubuhi na kubaki wazi hadi jioni kwa ajili ya kutoa nafasi kwa watu wengi zaidi wanaokuja kuangalia malikale zilizopo kwenye makumbusho hiyo.

Watu waliokuja kutembelea makumbusho ya Alkafeel wamepongeza malikale zilizopo na ustadi wa mpangilio wa makumbusho hiyo, unaoendana na utukufu wa turathi za kitamaduni na kidini.

Watu wengi wamekuja kutembelea makumbusho hii kutokana na nafasi yake katika kutunza turathi za kitamaduni na kidini kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: