Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imefanya nadwa yenye anuani isemayo (Nufaika na likizo ya kiangazi kwa kukuza kipaji cha mwanafunzi), kwa wanafunzi wa mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi katika mji wa Baabil.
Nadwa imeratibiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Baabil chini ya Majmaa.
Mhadhiri wa nadwa hiyo iliyofanywa wilaya ya Kuthi kaskazini ya mkoa wa Baabil ni Dokta Haidari Shilaa, nayo ni sehemu ya mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi zinazolenga kujenga kizazi cha wasomi wa elimu ya Qur’ani na kizazi kitakasifu.
Mradi wa semina za Qur’ani za majira ya kiangazi unalenga kufundisha misingi ya kiislamu kwa mujibu wa mafundisho ya vizito viwili, sambamba na kuendeleza vipaji vyao.