Ameyasema hayo alipompokea kiongozi wa kituo cha Aljuud Sayyid Ahmadi Twalibu Abdul-Amiir na watumishi wa kituo hicho, ambapo amesikiliza maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na kituo hicho na ushiriki wa mwisho kwenye kongamano la picha za katuni lililofanywa Baabil chini ya wizara ya utamaduni na utalii, na kongamano la sinema kimataifa awamu ya sita lililofanywa katika mji wa Kirkuuk, ambako kituo kilipata nafasi ya kwanza kupitia filamu ya (Ishi buibui), ambayo inamatukio ya kijana asiyefata nasaha za wazazi wake na anamfuata kijana muovu ikawa ni sababu ya kujiingiza kwenye matumizi ya daya za kulevya.
Sayyid Swafi amepongeza kazi zinazofanywa na kituo hicho, akahimiza ulazima wa kuendelea kutoa kazi zenye faida katika jamii na kupanua wigo wa kazi zake.
Kiongozi wa kituo cha Aljuud amesema “Tumekutana na Muheshimiwa Sayyid Swafi na kumuonyesha mafanikio ya kituo, ikiwa ni pamoja na tuzo tulizopata kwenye kongamano la sinema lililofanywa Kirkuuk na Baabil, amepongeza kazi zinazofanywa na kituo na mafanikio yake”.