Atabatu Abbasiyya imetoa mualiko kwa uongozi mkuu wa Masjidi Kufa.

Atabatu Abbasiyya imetoa mualiko kwa uongozi wa Masjid Kufa katika mkoa wa Najafu, kuja kushiriki kwenye wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya pili.

Mmoja wa watumishi wa idara ya mahusiano na mawasiliano ya ndani katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Sajjaad Hussein Khalf amesema “Kitengo kimepokea maagizo kutoka kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ya kutoa mialiko ya kushiriki kwenye wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya pili kwa taasisi za kidini, kielimu na kitamaduni hapa nchini ikiwemo Masjidi Kufa”.

Ataba inafanya kongamano la wiki ya Uimamu chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mwenendo wa Maimamu katika malezi ya mtu na umma) kuanzia tarehe (27/6/2024m hadi 4/7/2024m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: