Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetoa mualiko wa kuhudhuria wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya pili kwa chuo kikuu cha Misaan.
Atabatu Abbasiyya inafanya program ya wiki ya Uimamu kimataifa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu -a.s- katika kulea mtu na umma) kuanzia tarehe 27/6/2024m hadi 4/7/2024m.
Rais wa chuo dokta Aadil Maanii amesema “Watafiti wa chuo kutoka vitivo na vitengo tofauti wataenda kushiriki kwenye kongamano hilo” akasema kuwa “Chuo hushiriki kwenye makongamano mbalimbali ambayo huandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.