Atabatu Abbasiyya imetoa mualiko kwa uongozi mkuu wa Masjidi Sahlah.

Atabatu Abbasiyya imetoa mualiko kwa uongozi mkuu wa Masjidi Sahlah katika mkoa wa Najafu, kuja kushiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.

Mkuu wa kitengo cha Habari katika Masjid Sahlah Sayyid Luay Aljaburi amesema “Uongozi mkuu wa Masjid Sahlah umepokea mualiko wa Kwenda kushiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili katika Atabatu Abbasiyya, hivyo ujumbe wa Masjid Sahlah utakwenda kushiriki kwenye ratiba za wiki hiyo tukufu”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya imekua mstari wa mbele daima katika kuandaa ratiba zinazokusanya jamii na kutoa mafundisho ya Ahlulbait (a.s)”.

Atabatu Abbasiyya inafanya program ya wiki ya Imamu kwa mara ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: