Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, kinasafisha maeneo yote yanayozunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya sikukuu ya Idul-adh-ha.
Kiongozi wa idara ya usafi chini ya kitengo hicho Sayyid Muhammad Habiib Haadi amesema “Watumishi wa kitengo wanasafisha maeneo yote yanayozunguka Atabatu Abbasiyya baada ya maeneo hayo kushuhudia idadi kubwa ya mazuwaru katika siku za Idul-adh-ha”.
Akaongeza kuwa “Kazi hiyo imehusisha kusafisha eneo la mlango wa Qibla, sehemu inayozunguka Ataba tukufu, Barabara na mitaa inayoelekea kwenye malalo takatifu sambamba na kutupa taka zote zilizokuwa kwenye tenki za taka na kuzisafisha”.
Akasema “Watumishi wa Atabatu Abbasiyya hufanya juhudi kubwa katika kuhudumia mazuwaru wa malalo takatifu”.