Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya, wameweka mapambo yanayoashiria furaha kufuatia kukaribia kwa Idul-Ghadiir.
Rais wa kitengo Sayyid Khaliil Mahadi Hanuun amesema “Watumishi wa kitengo chetu wameanza kuweka mapambo yanayoashiria furaha, ambayo ni shada za mauwa, mabango yaliyoandikwa sifa za Imamu Ali bun Abuu Twalib (a.s) katika sehemu mbalimbali za Ataba tukufu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Idullahi-Akbaru”.
Akaongeza kuwa “Mapambo yanayo ashiria furaha yamewekwa kwenye kuta, milango ya Ataba na Barabara zinazoelekea kwenye haram tukufu”.
Akaendelea kusema “Watumishi wa kitengo hiki kwenye kila tukio la furaha, kama kuzaliwa kwa Imamu (a.s), sikukuu ya Idulfitri, Udh-ha na Idul-Ghadiir, hugawa marashi na mauwa kwa mazuwaru wanaokuja kutoa pongezi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.