Majmaa-Ilmi inafanya mradi wa (Wasomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu) awamu ya tatu katika wilaya ya Hindiyya.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu inafanya mradi wa (Wasomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu) wa kuhifadhi kwa haraka, awamu ya tatu katika wilaya ya Hindiyya mkoani Karbala.

Mradi huo unasimamiwa na Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Majmaa.

Kiongozi wa tawi la Hindiyya Sayyid Haamid Mar’abi amesema “Washiriki wa mradi huu ni wanafunzi (50), unafanyika kwa awamu ya tatu, tunawahifadhisha sura za Qur’ani kwa haraka kupitia njia za ufundishaji za kisasa bila kuathiri ufasaha katika usomaji”.

Akaongeza kuwa “Mradi unahusisha masomo ya Aqida, Fiqhi, Akhlaqi pamoja na masomo ya kuhifadhi kwa lengo la kuwajenga wanafunzi waweze kushikamana na vizito viwili”.

Akaendelea kusema “Katika awamu iliyopita wanafunzi walipata mafanikio mazuri, walihifadhi zaidi ya matarajio, mwaka huu tunajitahidi kupata mafanikio makubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: