Meja Jenerali Sayyid Ahmadi Niimatu-Swafi amesema “Kikosi cha Abbasi (a.s) kinashiriki katika kulinda misafara ya mahujaji kwa kushirikiana na vikosi vya Karbala, jeshi la muungano sambamba na kutoa huduma mbalimbali kwa mahujaji”.
Akaongeza kuwa “Miongoni mwa huduma zinazotolewa ni kugawa chakula, maji ya kunywa, huduma za afta, gari maalum 12 za kubeba wagonjwa zimeandaliwa”.
Akafafanua kuwa “Barabara inayolindwa na kikosi cha Abbasi (a.s) iko salama zaidi, kwani imefungwa kamera na kunakikosi maalum cha mafundi ambao wako tayari kutengeneza gari lolote litakalopata tatizo katikati ya safari”, akasema “Atabatu Abbasiyya imechangia upatikanaji wa gazi za kubeba mahujaji, chakula na huduma zingine”.