Mshauri wa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Faaiz Shakraji amesema “Warsha imehusisha kufundisha mbinu za kukaa na watu wenye umri mkubwa miongoni mwa mazuwaru, njia za kuamiliana nao na kuwapa mlo salama kwa afta zao”.
Akaongeza kuwa “Warsha imejikita katika kufafanua aina za maradhi wanayougua zaidi wazee, miongoni mwa maradhi hayo ni (matatizo ya mifupa na viungo) sambamba na kuwaelekeza aina ya mazowezi yanayo saidia mzunguko wa damu mwilini na mihadhara mingine”.
Ataba tukufu huimarisha uwezo wa watumishi wake kwa kufanya warsha na nadwa mbalimbali.