Kitengo cha kusimamia haram tukufu katika Atabatu Abbasiuyya, kinagawa pipi na mauwa kwa mazuwaru kufuatia kuingia kwa Idul-Ghadiir.
Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram wanagawa pipi na mauwa kwa mazuwaru wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kufuatia kuingia sikukuu ya Idul-Ghadiir.
Kwenye kila tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu mtakasifu (a.s) au sikukuu ya Idul-Fitri, Udh-ha na Ghadiir, kitengo cha kusimamia haram hugawa marashi, mauwa na pipi kwa mazuwaru wanaokuja kutoa pongezi kwa mwezi wa familia (a.s).