Majmaa-Ilmi inafanya semina ya Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika.

Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya inafanya semina ya Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini wenye asili ya Afrika.

Semina hiyo inafaywa katika mji wa Najafu chini ya Majmaa, kupitia mradi wa Qur’ani awamu ya nane kwa kushirikiana na Markazi Dirasaati Afriqiyya chini ya Atabatu Abbasiyya.

Mmoja wa watumishi wa idara ya Qur’ani katika Maahadi Shekhe Mahadi Albayati amesema “Semina itakuwa na masomo ya muda mfupi kwa muda wa miezi sita, kwa ushiriki wa wanafunzi (18) kutoka nchi tofauti za Afrika na itakuwa na hatua tatu”.

Akaongeza kuwa “Hatua ya kwanza wanafundishwa usomaji sahihi wa Qur’ani, hatua ya pili kanuni za usomaji na hatua ya tatu Ulumul-Qur’ani, Tafsiri, Sauti na Naghma”.

Akasema “Semina inalenga kuimarisha uwezo wa usomaji na ufundishaji wa Qur’ani katika jamii ya waafrika kwa kuandaa walimu wenye uwezo wa kufundisha Qur’ani kwa ufasaha katika nchi zao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: