Majmaa-Ilmi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeadhimisha sikukuu ya Idul-Ghadiir katika mji mkuu wa Baghdad.
Wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi Qur’ani katika Maahadi ya Qur’ani tawi la Baghdad chini ya Majmaa, wameshiriki kwenye hafla hiyo.
Hafla imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Ali Amiir, kisha mwanafunzi Muhammad Swadiq akasoma beti za mashairi kuhusu Idul-Ghadiir.
Hafla imepambwa na qaswida kutoka kwa wanafunzi na walimu wao, zilizo onyesha furaha kufuatia kumbikizi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipomtawalisha Imamu Ali bun Abutwalib (a.s) kuwa kiongozi wa waislamu kwa amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu.