Watu wa Karbala wanaadhimisha Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya Imamu Ali (a.s).

Maukibu ya watu wa Karbala imeadhimisha Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya Imamu Ali bun Abuutwalib (a.s).

Makamo rais wa kitengo cha maadhimishi na Mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Muhammad Twawiil amesema “Watu wa Karbala kwa kushirikiana na kitengo chetu wameadhimisha sikukuu ya Idul-Ghadiir mbele ya malalo ya Imamu Ali (a.s) katika mji wa Najafu”.

Akaongeza kuwa “Kitengo kimeandaa gari 50 kwa ajili ya kupeleka watu katika mji wa Najafu na kuwarudisha Karbala baada ya kumaliza maadhimisho yao ndani ya ukumbi wa Fatuma Zaharaa (a.s) katika Atabatu Alawiyya”.

Maukibu hiyo ni sehemu ya utamaduni wa watu wa Karbala kwa kushirikiana na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuadhimisha matukio ya Ahlulbait (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: