Atabatu Abbasiyya imeratibu ziara katika mji wa Samaraa kwa watu wenye asili ya Afrika.

Kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, kimeratibu ziara katika Atabatu Askariyya na malalo ya Sayyid Muhammad mtoto wa Imamu Haadi (a.s) kwa watu wenye asili ya Afrika.

Kiongozi wa idara ya tablighi katika Markazi Dirasaati Afriqiyya Sayyid Muslim Aljaabiri amesema “Ziara inalenga kujenga mafundamano ya kiroho na Ahlulbait (a.s) na kuwatambulisha Maimamu watakasifu (a.s) kwa waafrika”.

Akaomgeza kuwa “Ziara ilikuwa na vipengele vingi, wametambulishwa vitu mbalimbali na kusikiliza muhadhara kuhusu historia ya Maimamu na utukufu wao (a.s)”.

Akabainisha kuwa “Ziara hii ni sehemu ya kuimarisha uwelewa wa Dini kwa watu wenye asili ya Afrika waishio Iraq na kuimarisha mahusiano ya kijamii baina yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: