Chuo kikuu cha Misaan kimesema: Wiki ya Imamu imejikita kwenye mambo ya kimalezi yaliyofundishwa na Maimamu (a.s).

Rais wa chuo cha Misaan Dokta Aadil Maanii amesema kuwa, wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili imejikita kwenye mambo ya kimalezi yaliyofundishwa na Maimamu (a.s) katika kujenga misingi ya jamii.

Ameyasema hayo alipohudhuria wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili, inayosimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visitotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kuleo mtu na umma) kuanzia tarehe 27/6/2024m hadi 4/7/2024m.

Dokta Aadil amesema “Wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili imejikita kwenye mafundisho ya Maimamu (a.s) katika kuweka misingi bora ya jamii”, akaongeza kuwa “Watafiti wamewasilisha mada zinazoelezea nafasi ya Maimamu (a.s) katika mafundisho ya mtu na umma”.

Akaongeza kuwa “Atabatu Abbasiyya inaushirikiano mzuri na vyuo vikuu vya Iraq kwa kushiriki kwenye makongamano na harakati mbalimbali”.

Akasisitiza kuwa “Wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili inaonyesha nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika kutambulisha mafundisho ya Ahlulbait (a.s) kwenye kizazi cha sasa na kueneza muongozo uliotolewa na Maimamu (a.s) katika jamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: