Kuhitimisha kikao cha kielimu cha wiki ya Imamu kimataifa kwa lugha ya kiengereza

Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha kikao cha kielimu katika wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili kwa lugha ya kiengereza.

Atabatu Abbasiyya inafanya kongamano la Imamu kimataifa awamu ya pili, chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma).

Kongamano limehudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya, viongozi wa hauza na kisekula, jumla ya mada (18) zimejadiliwa kupitia vikao viwili cha asubuhi na jioni, miongoni mwa mada hizo ni, kulea nafsi, Akhlaqi, Jamii, Maadili ya kidini na kitamaduni na Afya katika mtazamo wa Ahlulbait (a.s).

Mwisho wa kikao hicho washiriki wakapewa zawadi zilizokabidhiwa kwao na mshauri wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Twalali Biiri, rais wa jumuiya ya Al-Ameed Dokta Riyadhi Twariq na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Hassan Daakhil.

Atabatu Abbasiyya inafanya kila iwezalo katika kuonyesha elimu ya Ahlulbait (a.s) na historia yao katika kutatua changamoto sambamba na kubainisha nafasi yao (a.s) katika kupambana na fikra potofu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: