Rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Yasiri amesema kuwa tafiti za kongamano la Sajjaad (a.s) zinaendana na mada zake.
Atabatu Abbasiyya inafanya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili chini ya kauli mbiu isemayo (Utume na Uimamu ni vitu viwili visivyotofautiana) na anuani isemayo (Mfumo wa Maimamu –a.s- katika kulea mtu na umma).
Akasema kuwa “Idadi ya tafiti zilizopokewa na kamati ya maandalizi zilikuwa (19), zilizokubalika ni (17) na zilizowasilishwa ni (7), mada zote zilizokubaliwa zitachapishwa kwenye jarida maalum”.
Akaongeza kuwa “Kongamano limepata muitikio mkubwa wa washiriki kutoka nchi tofauti, Aljeria, Moroko, Kuwait, Iran pamoja na mwenyeji Iraq”.
Akabainisha kuwa “Tafiti zilizowasilishwa kwenye kongamano la Imamu Sajjaad (a.s) zinaendana na mada zilizoandaliwa na kamati ya maandalizi”.
Kongamano hilo limesimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya, limehudhuriwa na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Abbasi Mussa Ahmadi, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya Ataba tukufu, viongozi wa idara, viongozi wa hauza na kisekula.