Ugeni kutoka Misri umetembelea makumbusho ya Alkafeel ndani ya Atabatu Abbasiyya.

Ugeni kutoka nchini Misri unaohusika na makumbusho, umetembelea makumbusho ya Alkafeel ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pembezoni mwa ratiba ya wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.

Wametembelea makumbusho hiyo kwa ajili ya kuangalia mali-kale zilizopo kwenye ukumbi wa makumbusho ndani ya Ataba tukufu, ugeni huo unawataalam wa mambo ya makumbusho wanaoshiriki kwenye wiki ya Imamu kimataifa awamu ya pili.

Wameangalia mali-kale zilizopo na namna ya utunzwaji wake.

Ziara hiyo inalenga kujenga ushirikiano baina yao, kwani Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi kubwa kuhakikisha makumbushi wa Alkafeel inakuwa jukwaa kubwa la watafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: